•Mheshimiwa huyo alikiri amejiondoa rasmi kwenye chama hicho cha UDA na atawania kiti hicho cha ugavana kama mgombeaji huru
Mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Kirinyaga, Purity Ngirichi siku ya Alhamisi alijiondoa rasmi kwenye chama cha UDA ambacho kinahusishwa na Naibu wa rais William Ruto.
Ngirichi alifichua hatua yake wakati alikuwa amezuru eneo Bunge la Mwea na Gichugu ambapo alikuwa anawapelekea wakazi chakula.
Aliwasuta maafisa wa chama cha UDA kwa kumwambia ajiondoe kwenye kinyang'anyiro cha kiti cha ugavana na badala yake awanie kiti cha ubunge cha Mwea, kwa tikiti ya chama hicho.
Mheshimiwa huyo alikiri amejiondoa rasmi kwenye chama hicho cha UDA na atawania kiti hicho cha ugavana kama mgombeaji huru
Mshirika huyo wa karibu wa Ruto, Ngirichi alikuwa alikuwa anakipia upato chama UDA hadi siku mpinzani wake wa kisiasa na Gavana wa Kirinyaga, Ann Waiguru alipojiunga rasmi na chama hicho walichokitengeneza.
Ngirichi aliwaambia wakazi wao ndio wako na usemi wa kuchagua,hivyo ifikiako siku ya uchaguzi wafanye maamuzi ya busara kwa sababu wao hawawezi kudanganywa wakati huu
"Mimi nasema hakuna mtu napendekeza, watu wa Kirinyaga ndio wana ajiri na ndio wanafuta "