COVID 19: Visa vipya 2, 127 vyarekodiwa, Vifo 3 vyaripotiwa

Muhtasari

•Habari njema ni kwamba wagonjwa 1, 434 wameweza kupata afueni, 1404 wakiponea nyumbani huku 30 wakiponea hospitali.

Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MAKTABA

Kenya imerekodi visa vipya 2, 127 ndani ya kipindi cha masaa 24 ambacho kimepita. Hii ni kutoka kwa sampuli 6, 710 ambazo ziliweza kupimwa.

Kiwango cha maambukizi kwa sasa kimesimamia 31.7%.

Mtoto wa miezi nane na mkongwe wa miaka 103 ni miongoni mwa wagonjwa wapya wa maradhi hayo.

Kufikia sasa Kenya imewahi kuripoti visa 297, 155 kutoka kwa sampuli 3, 036, 982 ambazo zimepimwa tangu janga la Corona lilipoingia nchini.

Nairobi inaendelea kuongoza kwa maambukizi huku leo ikiripoti visa 961. Nyeri ni ya pili na visa 120 huku Kericho ikifuata na via 104.

Habari njema ni kwamba wagonjwa 1, 434 wameweza kupata afueni, 1404 wakiponea nyumbani huku 30 wakiponea hospitali.

Vifo vitatu vimeripotiwa na kufikisha idadi ya walioangamizwa na virusi hivyo nchini kuwa 5, 381.

Wagonjwa 1,016 wanaendelea kupokea matibabu hospitalini huku wengine 23, 021 wakipokea matibabu nyumbani. Wagonjwa 39 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Chanjo ya Corona

Kufikia sasa jumla ya chanjo 10, 100, 993 zimepeanwa hapa nchini. Watu 5, 862, 875 wameweza kupokea angalau dozi moja ya chanjo huku 4, 206, 106 wakiwa wamepokea dozi zote mbili.