Kazi ya kusukuma wheelbarrow si kazi muhimu- Raila amrushia Ruto vijembe kuhusu kauli mbiu ya Hustler

Muhtasari
  • Raila amrushia Ruto vijembe kuhusu kauli mbiu ya Hustler
Kiongozi wa ODM Raila Odinga
Kiongozi wa ODM Raila Odinga
Image: MAKTABA

Kinara wa ODM, Raila Odinga siku ya Jumatatu alikosoa vikali Naibu wa rais William Ruto kwa  kauli mbio ya kazi ni kazi.

Bw Raila ambaye alitangaza wazi azma ya kuwania kiti cha urais kwa tiketi ya Azimio La Umoja, alikuwa anazungumza na wakazi wa eneo bunge la Lugari,  aliwahakikishia  kwamba  yeye ndiye ana uwezo wa kuendeleza nchi hii.

"Tumesema wale vijana wetu wamemaliza masomo, wapate kazi ya maana, ambayo inaweza peleka pesa mifukoni mwao, sio ati kazi ni kazi, kazi ya kusukuma 'wheerbarrow sio kazi" alisema Raila

Vile vile aliwaambia, zile pesa ambazo aliwahidi Ksh6000 akiingia mamkalani atahakikisha kila familia ambayo aina ajira itakuwa inapokea pesa hizo kila mwezi.  

"Ile jamii aina mapato yoyote itapata kwa  yangu serikali shilingi 6,000" Aliwauliza kama wanaunga mkono  pendekezo hilo lake na wote kwa pamoja wakakubali.

Alisema kuna mirengo inawaambia wananchi kuwa Baba anandanganya hakuna pesa atapeana akichukua hatamu ya uongozi, lakini aliwahahakishia kuwa yeye amekuwa waziri mkuu hivyo anajua mahali pesa hizo zitatoka.

"Wanasema ati Baba anandanganya watu ati hakuna pesa, nawambia ya kwamba Raila Odinga amekuwa waziri mkuu wa taifa la Kenya kwa miaka 5 najua pahali pesa ziko," Alizungumza Raila.