logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Shirika la reli larejesha safari za treni zilizositishwa

Shirika hilo  limesema huduma katika njia ya Nairobi- Madaraka-Pipeline-   Embakasi zinarejelewa  pamoja na  zinazopitia njia ya Nairobi- Kisumu-Limuru kuanzia Jumatatu, Januari 3, 2022

image
na

Habari03 January 2022 - 06:00
Mamlaka ya Keli ya Kenya

Shirika la reli siku ya jumapili lilitangaza safari za treni  kurejelewa baada ya kusitishwa kwa takribani siku 6.

Kupitia mtandao wa twitter Shirika hilo  limesema huduma katika njia ya Nairobi- Madaraka-Pipeline-   Embakasi  pamoja na  zinazopitia njia ya Nairobi- Kisumu-Limuru zitarejea kuanzia Jumatatu, Januari 3, 2022

"Tafadhali kumbukeni kuwa operesheni ya kawaida inaanza tena kesho, Januari, 3 kulingana na ratiba  ya kawaida iliyotolewa" shirika hilo lilinakiri kwa mtandao wake.

Shirika la Reli la Kenya lilipunguza huduma hizo sa usafiri wa Treni, mnamo Desemba 28, 2021  kufuatia idadi ndogo ya abiria iliyojitokeza wakati wa msimu wa sherehe za Krismasi na mwaka mpya. Mahitaji ya usafiri wa Treni yameanza kuongezeka  huku abiria wengi wakionekana kujitokeza.

Isitoshe Shirika hilo liliwahakikishia abiria kuwa nitaendelea kuwa hudumia kwa bei nafuu na ufanisi wa hali ya juu.

"Tunajitahidi kutoa salama, ufanisi wa kuaminika na kwa bei nafuu"


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved