Jamaa ajitoa uhai kwa kujikata kutumia msumeno jijini Nairobi

Muhtasari

•Inaripotiwa kwamba marehemu alijaribu kukata kichwa chake kutumia mashine hiyo alfajiri ya Jumanne.

crime scene
crime scene

Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 21 amejitoa uhai kwa kujikata kwa kutumia msumeno wa kukatia mbao katika mtaa wa Kasarani, kaunti ya Nairobi.

Inaripotiwa kwamba marehemu alijaribu kukata kichwa chake kutumia mashine hiyo alfajiri ya Jumanne.

Kijana huyo alikuwa amechukua mashine hiyo kutoka kwa karakana inayomilikiwa na babake kisha kwenda nayo nyumbani kwao ambapo aliitumia kujitoa uhai.

Mwili wa mtu huyo ulichukuliwa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti. Nia ya marehemu kuchukua hatua hiyo bado haijabainika.

Polisi walisema waliitwa katika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kisha kuupeleka hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.

Maafisa wa upelelezi jijini Nairobi wanasema wamegundua ongezeko la visa vya watu kujitoa uhai ambavyo vimekuwa vikiripotiwa kwao.

"Tunapokea ripoti za matukio kama haya karibu kila siku. Wengine wanashinikizwa na manmbo kama vile ugomvi wa kinyumbani na inatia wasiwasi,” alisema afisa wa polisi aliyehusika na uchunguzi wa matukio hayo.

Ripoti ya Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ilisema takriban watu 500 walijiua katika matukio tofauti katika kipindi cha miezi mitatu (Machi-Juni) ya 2021 nchini.