logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Makali ya corona: Watu 7 wameaga dunia huku 2,402 wakipatikana na virusi vya corona

Kwa habari za kuhuzunisha Watu 7 wameaga dunia kutokana na corona huku idadi ya walioaga ikifika 5,401.

image
na Radio Jambo

Habari04 January 2022 - 13:37

Muhtasari


  • Kati ya maambukizi hayo 2,098 ni wakenya huku 304 wakiwa raia wa kigeni,1,225 ni wanaume huku 1,177 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 302,134 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 22.6%

Watu 2402 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 nchini kutoka kwa sampuli 10,638 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 2,098 ni wakenya huku 304 wakiwa raia wa kigeni,1,225 ni wanaume huku 1,177 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 302,134 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 22.6%.

Mgonjwa wa chini ana umri wa miezi 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 104.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,056,954.

Vile vile watu 1,982 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 258,553, 1,929 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 53 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Kwa habari za kuhuzunisha Watu 7 wameaga dunia kutokana na corona huku idadi ya walioaga ikifika 5,401.

Kuna wagonjwa 1,124 ambao wamelazwa hospitalini, 25,631 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 50 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 10,220,981.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved