Mauaji ya kinyama Molo: polisi wasaka mwafunzi wa chuo kikuu

Kichwa chake kilikuwa kwenye ndoo katika chumba walichokuwa pamoja.

Muhtasari

Maafisa waliotembelea eneo la tukio walisema walipata kichwa cha msichana huyo kitandani huku mikono ikipatikana kwenye barabara iliyo karibu.  

Viungo vya mwili vilihamishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha eneo hilo.

Kichwa chake kilikuwa kwenye ndoo katika chumba walichokuwa pamoja.

Crime scene
Crime scene

Polisi huko Molo wanamsaka mwanafunzi wa chuo kikuu baada ya mpenzi wake kupatikana ameuawa na mwili kupatikana chumbani usiku wa kuamkia Jumatano.

Maafisa waliotembelea eneo la tukio walisema walipata kichwa cha msichana huyo kitandani huku mikono ikipatikana kwenye barabara iliyo karibu.  

Kichwa chake kilikuwa kwenye ndoo katika chumba walichokuwa pamoja. Chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika lakini polisi walisema wanataka kuzungumza na mshukiwa Mark Njoroge ambaye hajulikani aliko tangu kutokea kwa tukio hilo.  

Viungo vya mwili vilihamishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha eneo hilo.

Kwingineko,

Polisi wanachunguza mauaji ya mwanamume mwenye umri wa miaka 26 aliyepatikana amefariki katika nyumba ya kulala wageni huko Mlolongo, Kaunti ya Machakos.

Mwili wa Clinton Wanakacha ulipatikana ukiwa umetandazwa kwenye kitanda katika chumba cha sita, cha nyumba ya wageni ya Miathathia na wafanyikazi wa kituo hicho.

Mfanyakazi wa eneo hilo aliwaambia maafisa wa upelelezi kuwa marehemu alikuwa amekodisha chumba hicho Jumanne usiku akiwa na mwanamke ambaye bado hajatambulika.

Kondomu mbili zilizotumika zilipatikana wakati wapelelezi wakikagua chumbani humo, ili kupata vidokezo ambavyo vingesaidia kutambua kiini cha mauaji hayo. Mwili wake ulihamishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.