Muigizaji wa Zora Jackie Matubia atangaza ujauzito

Jackie Matubia AKA Nana
Jackie Matubia AKA Nana

Muigizaji wa Zora, Jackie Matubia almaarufu Nana   ametangaza wazi kuwa anatarajia mtoto wa pili. 

Jackie ambaye alikuwa muigizaji wa zamani wa kipindi cha Tahidi High  alipasua mbarika baada ya kuficha ujauzito  mwaka jana.

kupitia ukurusa wake wa  Instagram aliweka kanda  video yenye sauti ya kutoa nyoka pangoni huku akipasua habari hizo za ujauzito wake.Huku chini yake akinakiri maneno yakuvutia macho mashabiki wake

"Itabidi  mnihukumu juu siwezi  eleza...mtoto namba 2" Nana aliandika ujumbe chini ya video aliyokuwa kuwa amechapisha.

Habari hizo ziliwaacha mashabiki wake, hasa wa mitandao, wakiwa na furaha isiyofichika huku wakimpa hongera kwa ujauzito huo.

kwenye video hio,  anaonekana akipapasa ujauzito wake huku ikionekana  ni kama ako siku za mwisho za ujauzito huo kwa sauti yenye mvuto wa aina yake anasikika akisema "nilichukua  muda wa kupumzika na sasa ni wakati wa mtoto..."