Vinara wa Muungano wa One Kenya wanatarajiwa kuhutubia wanahabari Jumatano asubuhi kufuatia habari za kuongezeka kwa mpasuko wa muungano huo
Katibu wa One Kenya amesema kikao hicho na wanabahabari ambacho kimetabiriwa kufanyika mwendo wa saa 10 asubuhui kitahudhuriwa na vinara wote wa OKA
Vinara hao ni ikiwemo na Musalia Mudavadi wa ANC, Moses Wetang'ula wa Ford Kenya, Kalonzo Musyoka wa Wiper, Gideon Moi wa KANU.Cyrus Njirongo anatarajiwa kuhutubia umma pia
Mkutano huo wa dharura umeandaliwa baada ya Naibu Rais, William Ruto kuonekana akiwa na mpango wa kufanya kazi pamoja na baadhi ya vinara wa muungano wa OKA.
Isitoshe pia, kinara wa ODM, Bw Raila Odinga ameokana kwa ukaribu sana na seneta wa Baringo, Gideon Moi, ambaye siku ya mkutano wa Azimio la Umoja alihudhuria mkutano ulioandaliwa Kasarani wa Azimio la umoja
Baadhi ya vinara Ruto analenga kuwavuta kurtoka mrengo huo, ni ikiwemo na Musalia mudavadi na seneta Moses Masika Wetang'ula