logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Covid-19:Wagonjwa 25,024 wamejitenga nyumbani kutokana na corona,7 waaga dunia

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 306,686 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 22.1%.

image
na Radio Jambo

Habari06 January 2022 - 14:31

Muhtasari


  • Mgonjwa wa chini ana umri wa miezi 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 104
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,076,181
  • Kwa habari za kuhuzunisha Watu 7 wameaga dunia kutokana na corona huku idadi ya walioaga ikifika 5,411
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe akutana na Baraza la Magavana mjini Mombasa mnamo Desemba 15.

Watu 2,336 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 nchini kutoka kwa sampuli 10,558 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 2,029 ni wakenya huku 307 wakiwa raia wa kigeni,1,183 ni wanaume huku 1,153 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 306,686 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 22.1%.

Mgonjwa wa chini ana umri wa miezi 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 104.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,076,181.

Vile vile watu 1,759 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 261,067, 1,699 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 60 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Kwa habari za kuhuzunisha Watu 7 wameaga dunia kutokana na corona huku idadi ya walioaga ikifika 5,411.

Kuna wagonjwa 1,176 ambao wamelazwa hospitalini, 25,024 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 44 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 10,356,914.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved