Covid-19: Watu 14 wafariki kutokana na corona,2,444 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Kuna wagonjwa 1,208 ambao wamelazwa hospitalini, 26,324 wamejitenga nyumbani
  • Vile vile kuna wagonjwa 46 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)
  • Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 10,473,483
Image: HISANI

Visa 2,444 vipya vya maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini  kutoka kwa sampuli 9,269 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 2,298 ni wakenya huku 146 wakiwa raia wa kigeni,1,122 ni wanaume huku 1,322 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 309,130 na kiwango cha maambukizi cha asilimia  26.4%.

Mgonjwa wa chini ana umri wa miezi 3 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 110.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,085,450.

Vile vile watu 1,066 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 262,133, 1,016 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 50 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Kwa habari za kuhuzunisha Watu 14 wameaga dunia kutokana na corona huku idadi ya walioaga ikifika 5,425.

Kuna wagonjwa 1,208 ambao wamelazwa hospitalini, 26,324 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 46 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 10,473,483.