Mwalimu mstaafu,76,apatikana amefariki kwenye chumba cha wageni Molo

Muhtasari
  •  Mwanamme huyo, 76,  alipoteza maisha yake kwa njia isiyojulikana baada ya  kujivinjari na mwanamke moja    
  • Inasemekana  marehemu  alikuwa amebugia pombe ya kienyeji huko Miti Mirefu  kabla ya kwenda chumba hicho cha wageni. Baadaye   alijiunga na msichana wa  Twilight
crime scene
crime scene
Image: HISANI

Mwalimu mstaafu wa miaka 76  alipatakana amefariki katika chumba kimoja cha kulala wageni   Molo, kaunti ya Nakuru.

Hii ni baada ya kulala usiku  na mwanamke ambaye  alisafiri kabla ya kupambazuka.

Kitengo cha upelelezi wa Jinai (DCI),  Mwanamume huyo, 76, alipoteza maisha yake kwa njia isiyojulikana baada ya  kujivinjari na mwanamke moja.

Mwili wa mzee huyo ulikutwa ukiwa umetulia kwenye kitanda kwenye chumba alichokodi kwa ajili ya burudani.

Inasemekana  marehemu  alikuwa amebugia pombe ya kienyeji huko Miti Mirefu  kabla ya kwenda chumba hicho cha wageni. Baadaye   alijiunga na msichana wa  Twilight

Wakati  msafishaji  alikuwa anasafisha vyumba vingine  vya kulala aligundua mlango wa chumba hicho haukuwa umefungwa na alipoingia ndani alipata Mwili wa Mwanamme huyo ukiwa kwenye kitanda.

Mara moja alitaarifu Meneja, Bernard Kiarie ambaye alipiga ripoti kwa DCI ilioko eneo hilo .

 Kulingana na DCI tukio hilo limejiri baada ya  tukio lingine la aina hiyo lililotokea Mlolongo siku mbili zilizopita, ambapo maiti ilipatikana na  kando yake kulikuwa na  mipira kondumu iliyotumika.

Kutokana na ongezeko hilo humu nchini  DCI inawashauri wamiliki wa vyumba vya kulala kuwa wanarekodi  maelezo ya kila mtu anayefika kwenye vituo vyao kama ilivyo kwenye hati zao za vitambulisho vya kitaifa

Aidha, kikosi cha wapelelezi  kilifika kwenye eneo la tukio  na wamekusanya baadhi ya vitu muhimu zitakazo sababisha kukamatwa kwa mshukiwa.