Ruto amtakia Raila heri njema akiadhimisha miaka 77 ya Kuzaliwa

Muhtasari

• Naibu Rais William Ruto amemtumia Kinara wa ODM, Raila Odinga  ujumbe  wa kumtakia heri njema siku ya kuzaliwa

• Kupitia ukurusa wake wa Twitter,Ruto  amemtakia Kinara wa Azimio la Umoja  miaka mingi zaidi duniani.

kinara wa ODM Raila Odinga
kinara wa ODM Raila Odinga
Image: Hisani

Naibu Rais, William Ruto amemtumia Kinara wa wa ODM, Raila Odinga  ujumbe  wa kumtakia heri njema anapoadhimisha mwaka wa 77 tangu azaliwe.

Kupitia ukurusa wake wa Twitter,Ruto  amemtakia Kinara waziri huyo mkuu wa zamani miaka mingi duniani.

"Heri ya kuzaliwa Jacom. Ubarikiwe na  mengine  mengi. @RailaOdinga" Alinakiri Ruto

 

Raila anasherekea miaka 77 ya kuzaliwa. Viongozi mbali mbali wamemiminia ujumbe wa kumkatia heri njema siku ya kuzaliwa.

Ujumbe wa Naibu Rais umewashangaza wakenya, kwa sababu ni wiki mbili zilizopita ambapo Ruto alikuwa akisherekea siku ya kuzaliwa na Kinara wa ODM hakumtumia ujumbe wowote.