logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Covid-19: Watu 9 waaga dunia,741 wapatikana na corona,306 wapona

Mgonjwa wa chini ana umri wa miezi 3 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 100.

image
na Radio Jambo

Burudani09 January 2022 - 13:02

Muhtasari


  • Kwa habari za kuhuzunisha Watu 9 wameaga dunia kutokana na corona huku idadi ya walioaga ikifika 5,446
  • Kuna wagonjwa 1,244 ambao wamelazwa hospitalini, 26,220 wamejitenga nyumbani
  • Vile vile kuna wagonjwa 56 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)
Waziri Mutahi Kagwe

Visa 741 vipya vya maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini  siku ya Jumapili kutoka kwa sampuli 5,329 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 655 ni wakenya huku 86 wakiwa raia wa kigeni,368 ni wanaume huku 373 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 311,538 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 13.9%.

Mgonjwa wa chini ana umri wa miezi 3 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 100.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,099,482.

Vile vile watu 306 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 264,962, 239 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 67 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Kwa habari za kuhuzunisha Watu 9 wameaga dunia kutokana na corona huku idadi ya walioaga ikifika 5,446.

Kuna wagonjwa 1,244 ambao wamelazwa hospitalini, 26,220 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 56 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 10,593,638.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved