Afisa wa polisi ajipiga Risasi Mombasa

Muhtasari

Konstebo Jacob Masha alitumia bunduki yake aina ya G3 kujipiga risasi ndani ya nyumba yake Jumapili usiku.Chanzo cha tukio hilo bado hakijabainika.

Makumi ya maafisa wa polisi wamekufa kutokana na kujitoa uhai katika hali inayohusishwa na msongo wa mawazo kazini.

Konstebo Jacob Masha alitumia bunduki yake ya G3 kujipiga risasi ndani ya nyumba yake Jumapili usiku. Picha: KWA HISANI
Konstebo Jacob Masha alitumia bunduki yake ya G3 kujipiga risasi ndani ya nyumba yake Jumapili usiku. Picha: KWA HISANI

Afisa wa polisi alijua kwa kujipiga risasi kichwani na bunduki yake ya kazi katika makaazi ya polisi eneo la Makupa, Mombasa.

Konstebo Jacob Masha alitumia bunduki yake aina ya G3 kujipiga risasi ndani ya nyumba yake Jumapili usiku.Chanzo cha tukio hilo bado hakijabainika.

Polisi walisema walisikia mlio wa risasi kutoka kwa nyumba ya afisa huyo na walipokagua walikuta imefungwa kutoka ndani.

 Hapo ndipo walipovunja mlango na kumkuta afisa huyo mwenye umri wa miaka 32 akiwa amelala kwenye dimbwi la damu akiwa amejipiga risasi kidevuni na risasi ikatoka kwenye paji la uso. 

Mwili ulihamishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. Kamanda wa polisi wa Pwani Manasseh Musyoka alisema wanachunguza tukio hilo. Hili ni tukio la hivi punde la afisa wa polisi kujitoa uhai katika msururu unaohusishwa na masuala ya kisaikolojia. 

 Kitengo cha ushauri nasaha kimeanzishwa ndani ya huduma polisi ili kuwasaidia maafisa hao kusimamia mambo yao. 

Makumi ya maafisa wa polisi wamekufa kutokana na kujitoa uhai katika hali inayohusishwa na msongo wa mawazo kazini.