Barabara ya Lang'ata kufungwa kwa kipindi cha wiki moja

Muhtasari

•KeNHA imesema barabara hiyo itafungwa kati ya Januari 10 na Januari 15 ili kupatia nafasi ujenzi wa flyover ya T-Mall.

Thika-Road-Jam
Thika-Road-Jam
Image: MAKTABA

Shughuli za usafiri katika sehemu za barabara ya Lang'ata zitatatizika kwa kipindi cha siku sita zijazo.

Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu nchini Kenya  (KeNHA) imesema barabara hiyo itafungwa kati ya Januari 10 na Januari 15 ili kupatia nafasi ujenzi wa flyover ya T-Mall.

Watumizi wa barabara hiyo wataelekezwa kwa njia mbadala katika kipindi ambacho ujenzi utakuwa unaendelea.

KeNHA imesema kwamba kazi ya ujenzi itakuwa inaendelea usiku kati ya saa tatu jioni na saa kumi na moja asubuhi.

Image: KeNHA

Waendesha magari wamehimizwa kufuata mpango wa kudhibiti trafiki uliowekwa na kumakinika zaidi barabarani.