KPLC yatoa sababu za kupotea kwa umeme nchini

Muhtasari

•KPLC imetangaza  kupotea kwa stima katika maeneo mbalimbali ya nchi kufuatia kuanguka kwa minara kwenye njia ya umeme ya Kiambere-Embakasi.

Image: MAKTABA

Kampuni ya kusambaza umeme nchini (KPLC) imetangaza  kupotea kwa umeme katika maeneo mbalimbali ya nchi kufuatia kuanguka kwa minara ya nyaya za umeme ya Kiambere-Embakasi.

Kupitia taarifa iliotolewa kwa vyombo vya habari, KPLC imesema hitilafu hiyo  ambayo imesababisha kukatizwa kwa umeme katika maeneo mengi ya nchi ilitokea siku ya Jumanne mwendo wa saa tano kasorobo asubuhi.

Kampuni hiyo imehakikishia Wakenya kwamba wahandisi wao wanashughulikia suala hilo na taarifa zaidi zitatolewa baadae.

"Tumepoteza huduma za usambazaji wa umeme kwa sababu ya minara iliyoporomoka kwenye njia ya umeme ya Kiambere-Embakasi saa 10.45 asubuhi ya leo. Wahandisi wetu wanafanya kazi ya kurejesha usambazaji wa umeme. Taarifa kuhusu tukio hilo itatolewa kwa wakati ufaao" KPLC imesema..

Kufuatia hayo kampuni hiyo imewaomba radhi wateja wake kutokana na matatizo yaliyosababishwa.