Covid 19: Visa vipya 1, 175 vyaripotiwa, Wagonjwa 3,025 wapona

Muhtasari

•Mtoto aliyezaliwa siku mbili zilizopita ndiye mgonjwa mpya mdogo zaidi huku mgonjwa mzee zaidi akiwa mkongwe wa miaka 108.

•Watu 6, 134, 511 wameweza kupokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona huku 4, 644, 213 wakiwa wamepokea dozi zote mbili.

Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MAKTABA

Wizara ya afya nchini imetangaza visa vipya 1, 175 vya Covid-19 kutoka kwa sampuli ya watu 10, 073 walioweza kupimwa ndani ya kipindi cha masaa 24 ambacho kimepita.

Kiwango cha maambukizi kwa sasa ni 11.7%  huku jumla ya visa vilivyowahi kuripotiwa hapa nchini sasa ikifika  3,127, 480.

Mtoto aliyezaliwa siku mbili zilizopita ndiye mgonjwa mpya mdogo zaidi huku mgonjwa mzee zaidi akiwa mkongwe wa miaka 108.

Kaunti ya Nairobi imeripoti visa 459, Kisii 92, Mombasa 71 huku kaunti zingine zikiripoti visa chini ya 50.

Wagonjwa 3, 025 wameweza kupata afueni, 188 ambao walikuwa wamelazwa hospitalini huku 2, 837 wakiponea nyumbani.

Habari za kusikitisha ni kwamba vifo 3 kutokana na maradhi hayo vimeripotiwa. Jumla ya vifo vya Corona sasa imefika 5,472.

Kwa sasa wagonjwa 1, 146 wamelazwa hospitalini huku wengine 15, 829 wakipokea matibabu kutoka nyumbani. Wagonjwa 49 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Chanjo ya Corona

Kenya imeweza kuchanja watu 10, 878, 311. Watu 6, 134, 511 wameweza kupokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona huku 4, 644, 213 wakiwa wamepokea dozi zote mbili.