Itumbi azungumzia mateso aliyopitia mikononi mwa watekaji nyara

Muhtasari

• Akizungumza siku ya Alhamisi, Itumbi alisema wanaume sita waliokuwa wamemteka nyara walikuwa na zamu ya kumpiga na kumfanyia madhila. 

• Alisema kuwa watu waliokuwa kwenye magari mawili walimtupa msituni akiwa uchi kabla ya kuondoka.

Mwanablogu Dennis Itumbi aliruhusiwa kutoka hospitalini
Mwanablogu Dennis Itumbi aliruhusiwa kutoka hospitalini
Image: HANDOUT

Mwanablogi Dennis Itumbi amesimulia masaibu yake ya uchungu mikononi mwa watu wanaodaiwa kumteka nyara. 

Akizungumza siku ya Alhamisi, Itumbi alisema wanaume sita waliokuwa wamemteka nyara walikuwa na zamu ya kumpiga na kumfanyia madhila. 

"Kikosi cha Hit Squad ambacho kinaendesha oparesheni zake kwa hofu ya kuonekana, kufichuliwa au kuonyeshwa hadharani, kilikuwa tayari kimeacha gari aina ya Premio walilokuwa nalo wakati nikitekwa katika eneo la Thindigua nje ya Kinyozi.

Wanaume sita walikuwa wanabadilishana zamu ya kunipiga na kifaa kama nyundo na silaha zingine," alisema. Alisema watekaji nyara aliowataja kuwa ni 'maofisa wa polisi wakorofi' walimtaka abadili msimamo wake wa kisiasa, lakini alikataa.

 "Lazima ubadilishe msimamo wako wa kisiasa kuendana na wa bosi," Itumbi alisema. “Yeyote yule, mwambie hatubadili imani yetu ya kisiasa, kwa nguvu na vitisho, inabidi ajifunze ujuzi wa kushawishi,” alijibu. 

Alisema kuwa watu waliokuwa kwenye magari mawili walimtupa msituni akiwa uchi kabla ya kuondoka.

 "Sikiza wewe, hatujakuua...lakini ukipiga nduru tutarudi tukumalize...." Itumbi narrated.

 "Mvua ilikuwa ikinyesha sana huku wakiendesha magari mawili. Nyeusi na nyeupe." 

Mwanablogu huyo alitekwa nyara alipokuwa akitoka kwenye kinyozi na kudaiwa kuteswa baadaye kabla ya kutupwa katika eneo la Lucky Summer, Kasarani, Nairobi. Alikuwa amevunjika mkono na miguu yake ilijeruhiwa kidogo baada ya kugongwa na nyundo. 

Baadaye Itumbi alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi hospitalini baada ya kupatikana na nimonia.

Naibu Rais William Ruto alidai kuwa Itumbi aliteswa na watu ambao walipaswa kumlinda.Polisi walikanusha kuhusika na tukio hilo baada ya wanasiasa washirika wa UDA kuwahusisha na kutekwa kwake. Msemaji wa polisi Bruno Shioso alisema wanachunguza tukio hilo.