Raila azindua miradi ya maji Taita -Taveta

Muhtasari

• Kiongozi huyo wa muungano wa Azimio la Umoja atazindua rasmi miradi mbali mbali ya maji iliyofadhiliwa na serikali ya kaunti ya Taita Taveta. 

• Raila atahutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya Overseer na Mwatate.

 

kinara wa ODM Raila Odinga
kinara wa ODM Raila Odinga
Image: Hisani

  Kinara wa Odm Raila Odinga ameanza ziara yake katika kaunti ya Taita Taveta. Raila anafanya ziara ya siku moja katika kaunti hiyo. 

Kiongozi huyo wa muungano wa Azimio la Umoja akiwa katika ziara hiyo atazindua rasmi miradi mbali mbali ya maji iliyofadhiliwa na serikali ya kaunti ya Taita Taveta. 

Waziri mkuu huyo wa zamani atafanya mkutano wa barazani ambapo atauza sera zake na kunadi muungano wa Azimio la umoja.

Katika mkutano huu atakutana na makundi mbali mbali kutoka kaunti ya Taita Taveta.  Miradi ya maji inayozinduliwa inapatikana katika maeneo ya Maktau na Overseer.

Maeneo haya yamekuwa yakikabiliwa na changomoto za maji tangu jadi na miradi hii ni afueni kubwa kwa wenyeji. 

Raila atahutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya Overseer na Mwatate. Katika hotuba yake anatarajiwa kuhubiri ujumbe wa amani, upendo, matumaini na ufanisi chini ya kampeini zake za Azimio la Umoja. 

Katika ziara hiyo Raila anaandamana na wenyeji wake Gavana Granton Samboja, Mbunge wa Mwatate Andrew Mwadime, Naibu kinara wa wengi bungeni Naomi Shaban, Seneta wa Taita-Taveta Jones Mwaruma miongoni mwa viongozi wengine.