UDA yadai uchunguzi juu ya machafuko yaliyoharibu mkutano wa DP Ruto Jacaranda

Muhtasari
  • UDA yadai uchunguzi juu ya machafuko yaliyoharibu mkutano wa DP Ruto Jacaranda
UDA yadai uchunguzi juu ya machafuko yaliyoharibu mkutano wa DP Ruto Jacaranda
Image: Mercy Mumo

UDA imemshutumu Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiangi kwa kuwa mpole sana katika kuchukua hatua dhidi ya wahusika wa ghasia za Jumapili kwenye mkutano wa naibu rais William Ruto huko Jacaranda, Nairobi.

Katibu mkuu Veronica Maina alisema Matiangi amefumbia macho machafuko hayo kwa sababu anaunga mkono azma ya kinara wa ODM Raila Odinga kuwania urais.

Chama hicho kinashutumu ODM kwa kuanzisha ghasia zilizoshuhudiwa katika hafla hiyo.

"Matiangi amemuunga mkono Raila hadharani. Tunamwomba avue kofia ya kisiasa na kuwaokoa Wakenya kutokana na kutovumiliana kisiasa. Wizara yake imesalia kimya kuhusu suala hilo lakini imechukua hatua haraka katika matukio mengine," Maina alisema.

Mwenyekiti wa chama cha UDA Johnson Muthama alilaumu Orange Democratic Movement (ODM) katika taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Jumatatu, akidai kuwa kundi hilo la kurusha mawe lilikuwa kwenye orodha ya malipo ya ODM.

"Tukio sawia na hilo lilitokea Kitale ambapo wabunge washirika wa UDA walikatizwa na polisi kufanya mkutano wa amani," Muthama alisema.

Hii si mara ya kwanza matukio haya mabaya kutokea. Mnamo Septemba 5, 2021, katika Kaunti ya Kieni Nyeri, msafara wa Naibu Rais ulipigwa mawe na miezi miwili baadaye katika shambulio kali zaidi, msafara wa Naibu Rais ulipigwa mawe Kondele Kaunti ya Kisumu. tarehe 10 Oktoba 2021."

 

 

 

 

UDA yadai uchunguzi juu ya machafuko yaliyoharibu mkutano wa DP Ruto Jacaranda
Image: Mercy Mumo
UDA yadai uchunguzi juu ya machafuko yaliyoharibu mkutano wa DP Ruto Jacaranda
Image: Mercy Mumo