logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Wacheni mucene!" Gavana Mutua azungumzia madai ya kupata kipenzi kipya baada ya kutengana na Lilian

Picha iliyokuwa inasambazwa mitandaoni ya kijamii siku ya Jumamosi ilizua gumzo kubwa huku baadhi ya wanamitandao wakiamini kuwa gavana huyo hatimaye ameponya jeraha lake la moyo na kutafuta mridhi wa Lilian.

image
na Radio Jambo

Makala16 January 2022 - 18:07

Muhtasari


•Picha iliyokuwa inasambazwa mitandaoni ya kijamii siku ya Jumamosi ilizua gumzo kubwa huku baadhi ya wanamitandao wakiamini kuwa gavana huyo hatimaye ameponya jeraha lake la moyo na kutafuta mridhi wa Lilian.

Gavana wa Machakos Alfred Mutua wakati wa uzinduzi wa manifesto yake ya Urais katika hoteli ya Panafric, Nairobi mnamo Desemba 5, 2021.

Gavana wa Machakos Alfred Mutua amepuuzilia mbali madai kwamba tayari amesonga mbele na maisha na kujinyakulia kipenzi kingine miezi kadhaa tu baada ya kutengana na aliyekuwa mpenzi wake Lilian Ng'ang'a.

Hii ni baada ya picha inayomuonyesha mwanasiasa huyo akiwa pamoja na mwanadada fulani asiyejulikana kuibuka kwenye mitandao ya kijamii.

Huku akijitetea kupitia ukurasa wake wa Instagram Mutua amedai kuwa mwanadada huyo ni mmoja tu wa watu wengi asiowajua ambao huomba kupiga naye picha kila wanapokutana.

"Ninaombwa kila siku na watu wengi kupiga picha. Nakubali kwa unyenyekevu. Ninapiga picha na watu nisiowajua - wanaume, wanawake, vikundi, watoto, familia n.k. Kwa kawaida wao huchapisha picha hizo." Mutua aliandika.

Picha iliyokuwa inasambazwa mitandaoni ya kijamii siku ya Jumamosi ilizua gumzo kubwa huku baadhi ya wanamitandao wakiamini kuwa gavana huyo hatimaye ameponya jeraha lake la moyo na kutafuta mridhi wa Lilian.

Alfred Mutua akiwa na mwanadada asiyejulikana

Mgombeaji huyo wa kiti cha urais katika chaguzi zijazo ameeleza kwamba kuonekana kwake pamoja na watu fulani hakumaanishi kuna uhusiano wowote kati yao.

"Hii haimaanishi nawajua au niko na biashara au urafiki nao. Wacheni mucene!" Mutua amesema.

Gavana huyo na aliyekuwa mpenziwe Lilian Ng'ang'a walitangaza kutengana kwao mnamo mwezi Agosti mwaka jana baada ya kuwa pamoja kwa kipindi cha takriban mwongo mmoja.

Bi Ng'ang'a tayari amenyakuliwa na mwanamuziki Julius Owino almaarufu kama Juliani huku Mutua akionekana kusalia kimya kuhusu maendeleo yake ya kimahusiano kufuatia utengano huo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved