Watu 5 wamefariki, watatu wajeruhiwa katika ajali ya barabara kuu ya Namanga-Kajiado

Muhtasari
  • Watu 5 wamefariki, watatu kujeruhiwa katika ajali ya barabara kuu ya Namanga-Kajiado
  • Miili ya marehemu imehamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kajiado, huku waliojeruhiwa wakilazwa katika kituo kimoja
Ajali
Ajali
Image: HISANI

Watu watano walipoteza maisha yao Jumamosi asubuhi baada ya magari mawili kugongana kwenye barabara kuu ya Namanga-Kajiado.

Polisi walisema wengine watatu waliachwa katika hali mbaya baada ya ajali hiyo katika eneo la Ilbisi.

Magari hayo yalikuwa yakielekea pande tofauti wakati wa ajali hiyo.

Probox, iliyokuwa ikielekea Ilbisil ilikuwa na watu kadhaa na wanne kati yao walikufa papo hapo huku wengine wakipata majeraha mabaya, polisi waliotembelea eneo la tukio walisema.

Miili ya marehemu imehamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kajiado, huku waliojeruhiwa wakilazwa katika kituo kimoja.

Polisi walisema wanachunguza tukio hilo.

Imejiri wakati ambapo maafisa wanasema ajali hizo zinaongezeka ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana tangu mwaka mpya.

Kufikia sasa zaidi ya watu 270 wameuawa katika ajali tangu mwaka mpya, kamanda wa trafiki Mary Omari alisema ikilinganishwa na 201 waliofariki kipindi kama hicho mwaka wa 2021.

Wengi wao ni watembea kwa miguu.