Mwanafunzi wa chuo kikuu akamatwa kwa kuuza mitihani ya KCPE na KCSE

Mshukiwa aliwadai watahiniwa shilingi 1,600 - 2,600 kwa mitihani tofauti

Muhtasari

•Brighton alipatikana na na karatasi bandia za mitihani hiyo huku akiwa amehifadhi zingine kwenye simu yake ya mkono.

Image: TWITTER// DCI

Wapepelezi wa DCI wamemtia mbaroni mwanafunzi wa ekonomia katika chuo kikuu cha Zetech kwa madai ya kuuza mitihani bandia ya KCPE na KCSE.

Kupitia taarifa iliyotolewa Ijumaa asubuhi, DCI imesema Oscar Brighton ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu alikamatwa Alhamisi na maajenti wa KNEC baada ya kuhusishwa na uhalifu huo.

Brighton alipatikana na na karatasi kadhaa bandia za mitihani hiyo huku akiwa amehifadhi zingine kwenye simu yake ya mkono.

Kulingana na DCI, mshukiwa alikuwa ameunda vikundi vya WhatsApp ambapo alikuwa anaendeleza biashara hiyo laghai.

Mshukiwa aliwadai watahiniwa shilingi 1,600 - 2,600 kwa mitihani tofauti. 

Brighton ambaye si mhalifu wa mara ya kwanza anatarijiwa kufikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kukiuka sheria za mitihani ya kitaifa.