Jamaa atiwa mbaroni kwa kuvamia polisi mwanamke na kuiba sare yake Mombasa

Muhtasari

•Mshukiwa alikamatwa katika eneo la Makupa na sare ya polisi iliyoibiwa kutoka kwa afisa huyo wa kike ikapatikana kwake.

crime scene 1
crime scene 1
Image: HISANI

Polisi jijini Mombasa wanamzuilia mshukiwa mmoja wa ujambazi aliyemvamia na kumpora polisi mwanamke sare yake na vitu vingine vya thamani.

Mshukiwa alikamatwa katika eneo la Makupa na sare ya polisi iliyoibiwa kutoka kwa afisa huyo wa kike ikapatikana kwake.

Tukio hilo lilitokea katika eneo la Changamwe takriban wiki moja iliyopita.

Polisi wanasema wanaendelea kuwasaka washukiwa zaidi waliohusika kwenye tukio hilo la wizi ambalo lilitokea wakati afisa huyo alikuwa akielekea kwenye kituo cha basi ili kuenda kazini.

Mshukiwa huyo alitarajiwa mahakamani kujibu mashtaka mbalimbali yakiwamo ya wizi wa kutumia nguvu.