logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ruto aachia wimbo wa 'hatupangwingwi' baada ya NCIC kupiga marufuku neno hilo

Ruto ameachia wimbo wa 'hatupangwingwi' saa chache baada ya NCIC kupiga neno hilo marufuku.

image
na Radio Jambo

Habari08 April 2022 - 12:07

Muhtasari


• Naibu rais William Ruto sasa ameachia kibao kwa jina ’hatupangwingwi’.

• Ruto, ambaye alikuwa amekumbatia msemo huo kama kaulimbiu yake katika kampeni, alipakia wimbo huo katika mitandao yake ya Twitter na Facebook siku ya Ijumaa.

 

Saa chache baada ya tume ya NCIC kupiga marufuku matumizi ya neno ‘sipangwingwi’ kwa kile walichokitaja kuwa linaeneza chuki, naibu rais William Ruto sasa ameachia kibao kwa jina ’hatupangwingwi’.

Ruto, ambaye alikuwa amekumbatia msemo huo kama kaulimbiu yake katika kampeni, alipakia wimbo huo katika mitandao yake ya Twitter na Facebook siku ya Ijumaa.

Naibu rais alikuwa ameshirikishwa kwenye wimbo huo na msanii E-xray.

NCIC Ijumaa iliorodhesha msemo ‘sipangwingwi’ kama moja ya kauli ambazo zinaeneza chuki miongoni mwa wakenya hasahasa katika kipindi hiki taifa linajiandaa kwa uchaguzi mkuu.

Maneno mengine ambayo yalitajwa na NCIC madoadoa, kama mbaya mbaya, oparesheni linda kura, ua, ufukizo.

Mwenyekiti wa NCIC Samuel Kobia alisema maneno hayo yamepigwa marufuku katika mikutano ya hadhara, kwenye mitandao ya kijamii na vipindi vya kisiasa.

“Hatua hii itasaidia pakubwa kuthibiti kauli za kueneza chuki na kuhakikisha taifa linashuhudia amani katika kipindi hiki cha uchaguzi.

 

 

 



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved