Polisi wanne watiwa mbaroni kwa madai ya ufisadi

Muhtasari

•Walijifanya maafisa kutoka Mamlaka ya Kukusanya Ushuru (KRA) na NEMA kisha kutumia fursa hiyo kutekeleza uhalifu wa ufisadi katika mtaa wa Ongata Rongai.

Pingu
Image: Radio Jambo

Maafisa wanne kutoka kituo cha polisi cha Kamukunji wapo kizuizini baada ya kukamatwa kwa madai ya ufisadi.

Oburo, Dorcas Nzilani na Winfred Kanana wanaripotiwa kutelekeza majukumu yao na kujifanya maafisa kutoka Mamlaka ya Kukusanya Ushuru (KRA) na NEMA kisha kutumia fursa hiyo kutekeleza uhalifu wa ufisadi katika mtaa wa Ongata Rongai.

Kitengo cha DCI kimeripoti kwamba, washukiwa, bila idhini yoyote waliondoka kituoni na kuenda kukamata wafanyibiashara wawili kwa madai ya kuwa na karatasi za plastiki.

Maafisa hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi huku uchunguzi zaidi ukiendelea kabla yao kuadhibiwa.