Spika wa bunge la Nairobi Benson Mutura kukesha katika seli za polisi

Muhtasari

• Siku ya Alhamisi alihojiwa kwa saa kadhaakatika makao makuu ya DCI kwa madai ya kumuibia muajiri wake kwa kuitisha marupurupu ya usafiri na ilhali hakusafiri.  

• Mutura aliandamana na wakili wake alipoelekea katika makao makuu ya DCI mwendo wa saa tano mchana na kuhojiwa kwa takriban saa tano. 

• Siku ya Jumatano Mutura alidai kwamba masaibu yake yalianza pale aliposema kwamba Nairobi Metropolitan Services ni taasisi haramu. 

Spika wa Bunge la Kaunti ya Nairobi Benson Mutura akiongoza kikao cha mawasilisho mnamo Oktoba 26, 2021 katika vyumba vya bunge. Picha: FI
Spika wa Bunge la Kaunti ya Nairobi Benson Mutura akiongoza kikao cha mawasilisho mnamo Oktoba 26, 2021 katika vyumba vya bunge. Picha: FI

 Spika wa bunge la kaunti ya Nairobi Benson Mutura atalazimika kukesha katika seli za polisi.  

Mutura ambaye anakabiliwa na tuhuma za wizi atalala katika kituo cha polisi cha Muthaiga akisubiri kufikishwa mahakamani.  

Siku ya Alhamisi alihojiwa kwa saa kadhaakatika makao makuu ya DCI kwa madai ya kumuibia muajiri wake kwa kuitisha marupurupu ya usafiri na ilhali hakusafiri.  

Pia anakabiliwa na kosa la kuchukuwa kitambulisho cha afisa mmoja wa polisi aliyekwenda kumkamata siku ya Jumatano katika jumba la City Hall. 

Mutura aliandamana na wakili wake alipoelekea katika makao makuu ya DCI mwendo wa saa tano mchana na kuhojiwa kwa takriban saa tano. 

Siku ya Jumatano Mutura alidai kwamba masaibu yake yalianza pale aliposema kwamba Nairobi Metropolitan Services ni taasisi haramu. 

"Kama ilivyo kwa sasa, NMs ni shirika lisilo halali kwani kuongezwa muda wake kuhudumu hakukufuata sheria," alibainisha. 

Mutura, ambaye ni mbunge wa zamani wa Makadara alidai kwamba hatua ya kuongeza muda wa NMS ilifaa kuidhinishwa na bunge la kaunti.