KODI

KRA: Usingojee siku ya mwisho, jaza kodi yako ya 2021

Ikiwa wewe ni mwajiri ambaye hajatoa fomu za P9, hii ni hamasisho kwako kuwapa wafanyikazi wako fomu zao za P9 kabla ya kuchelewa sana

Muhtasari
  • Unaweza kutembelea ofisi ya KRA iliyo karibu na wewe na kuomba msaada katika kujaza kodi yako.
  • Unda wakati katika ratiba yako ili kuwasilisha mapato yako na kulipa kodi yoyote ambayo hujalipa.

Kenya Revenue Authority (KRA) imewahimiza Wakenya kujaza kodi kabla ya tarehe ya mwisho ya Juni 30, 2022.

Msimu wa kufunguliwa kujaza kodi unaanzia Januari hadi Juni kila mwaka, kwa hivyo usisubiri hadi dakika ya mwisho kuwasilisha mapato yako. Kumbuka ni haki yako kudai fomu yako ya P9 mapema.

Ikiwa wewe ni mwajiri ambaye hajatoa fomu za P9, hii ni hamasisho kwako kuwapa wafanyikazi wako fomu zao za P9 kabla ya kuchelewa sana. Kushindwa kufanya hivyo  kabla ya siku ya mwisho kutavutia faini ya 2000 kwa wafanyikazi hao.

Unda wakati katika ratiba yako ili kuwasilisha mapato yako na kulipa kodi yoyote ambayo hujalipa.

Unaweza kutembelea ofisi ya KRA iliyo karibu na wewe na kuomba msaada katika kujaza kodi yako.

Pia unaweza piga simu kwa kituo cha mawasiliano kwenye 020 4 999 999 au 0711 099 999 au utume barua pepe callcentre@kra.go.ke kama unataka usaidizi wowote.

Watu wanaofaa kujaza kodi ya mwaka wa 2021

  1. Wakenya wasio na mapato/ajira wanafaa kujaza nil returns kwenye itax.
  2. Walipa kodi walio na cheti cha Kodi ya zuio
  3. Wakaazi wa kigeni wenye biashara nchini Kenya
  4. Wakenya walio ugenini
  5. Wafanyakazi wa Serikali ya Kaunti
  6. Watumishi wa umma
  7. Wakenya ambao wameajiriwa

Kamishna Jenerali wa KRA Githii Mburu akizungumzia suala la kulipa kodi mwaka jana alisema kwamba

lengo lao ni kufikisha Sh1.78 trilioni kwa kodi iliyolipwa. Kukabiliana na ukwepaji wa kodi na biashara haramu kwa sasa ni vipaumbele vya KRA kufikisha lengo hilo.

Fuata kurasa za media ya kijamii za KRA kwa habari zaidi:  Facebook: Kenya Revenue Authority, Twitter: KRACare, IG: KRA_Care

Skiza Tubonge tax Podcast  ifuatayo kupata maelezo zaidi: https://anchor.fm/storizaushuru/episodes/Filing-2021-Income-Tax-Returns-Part-3-Other-Sources-of-Income-with-Benson-Kakuno-e1h1ptv