Moja kwa moja: Uhuru aongoza taifa katika kutazama mwili wa hayati Mwai Kibaki

Muhtasari

• Hafla ya kutazama mwili wa marehemu rais mustaafu Mwai Kibaki itachukuwa siku tatu. 

• Marehemu Kibaki atazikwa siku ya Jumamosi nyumbani kwake Othaya. 

Rais mustaafu Mwai Kibaki alifariki siku ya Ijumaa wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 90.

Alikuwa rais wa awamu ya tatu wa Kenya baada ya kuchukuwa usukani kutoka hayati rais Daniel Moi. 

Marehemu Kibaki atazikwa siku ya Jumamosi nyumbani kwake Othaya.