Mwili wa aliyekuwa rais Mwai Kibaki wawasili katika majengo ya bunge

Muhtasari

• Msafara uliyobeba mwili wa rais wa tatu wa Kenya uliwasili katika majengo ya Bunge Jumatatu dakika chache kabla ya saa moja unusu asubuhi.

• Mwili wa rais huyo wa zamani wa Kenya utalala-bungeni kwa muda wa siku tatu zijazo.

Mwili wa Rais Mstaafu Mwai Kibaki ukiingizwa katika majengo ya bunge Aprili 25, 2022. Picha: EZEKIEL AMING'A
Mwili wa Rais Mstaafu Mwai Kibaki ukiingizwa katika majengo ya bunge Aprili 25, 2022. Picha: EZEKIEL AMING'A

Mwili wa aliyekuwa Rais Mwai Kibaki tayari umewasili katika majengo ya bunge.

Msafara uliyobeba mwili wa rais wa tatu wa Kenya uliwasili katika majengo ya Bunge Jumatatu dakika chache kabla ya saa moja unusu asubuhi.

Mwili huo ulisafirishwa kwenye msafara wa heshima uliongozwa na idara ya jeshi kutoka chumba cha kuhifadhia mati cha Lee Funeral Home na kuelekea Valley Road na Kenyatta Avenue kupitia Parliament Road.

Guaride ya Heshima ya Kijeshi iliwekwa kando ya Barabara ya Bunge kwa ajili ya msafara kuingia Bungeni.

Mwili wa rais huyo wa zamani wa Kenya utalala-bungeni kwa muda wa siku tatu zijazo.

Kibaki alifariki akiwa na umri wa miaka 90.

Mwili wa aliyekuwa Rais Mwai Kibaki uliwasili katika majengo ya bunge dakika chache kabla ya saa moja unusu asubuhi. Picha: EZEKIEL AMING'A
Mwili wa aliyekuwa Rais Mwai Kibaki uliwasili katika majengo ya bunge dakika chache kabla ya saa moja unusu asubuhi. Picha: EZEKIEL AMING'A
Mwili wa Rais Mstaafu Mwai Kibaki ukiwa bungeni Aprili 25, 2022. Picha: EZEKIEL AMING'A
Mwili wa Rais Mstaafu Mwai Kibaki ukiwa bungeni Aprili 25, 2022. Picha: EZEKIEL AMING'A
Mwili wa Rais Mstaafu Mwai Kibaki ukiwasili bungeni Aprili 25, 2022. Picha: EZEKIEL AMING'A
Mwili wa Rais Mstaafu Mwai Kibaki ukiwasili bungeni Aprili 25, 2022. Picha: EZEKIEL AMING'A