logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kibaki ndiye rais bora zaidi Kenya kuwahi kuwa naye, Uhuru ni mwanafunzi wake mzuri- Ruto asema

Rais Uhuru Kenyatta amejifunza mengi kutoka kwa Kibaki- Ruto

image
na

Yanayojiri29 April 2022 - 12:01

Muhtasari


•Ruto alisema Kibaki alikuwa mtumishi wa umma aliyeheshimika sana katika serikali na upinzani.

•Alisema kuwa hana shaka kuwa atakayekuwa rais wa tano ana maono sawa na atatafuta kuendeleza urithi wa KIbaki.

Naibu Rais William Ruto akitoa hotuba yake katika hafla mazishi ya kitaifa ya hayati Mwai Kibaki katika uwanja wa Nyayo mnamo Aprili 29, 2022

Naibu Rais William Ruto amemsifu marehemu Rais Mwai Kibaki na kumtaja kuwa rais bora zaidi Kenya kuwahi kuwa naye.

Akitoa hotuba yake katika hafla ya mazishi ya kiserikali iliyofanyika Jumamosi katika Uwanja wa Nyayo, Ruto alisema Kibaki alikuwa mtumishi wa umma aliyeheshimika sana katika serikali na upinzani.

"Yeye ni mwana mkubwa wa nchi yetu. Tunasherehekea mafanikio yake, mchango wake na urithi wake mzuri na thabiti," Ruto alisema.

Ruto alisema Kibaki alitoka katika mandhari duni katika kijiji cha Othaya ambako alikuwa akichunga mbuzi na kuwa kiongozi mkubwa, jambo ambalo viongozi wengine wamejifunza mengi kutoka kwake.

"Rais wa nne wa Kenya, Rais Uhuru Kenyatta amejifunza mengi kutoka kwake. Kenyatta amekuwa mwanafunzi mzuri wa rais Mwai Kibaki, najua kama naibu wake," Ruto alisema huku akishangiliwa sana.

Alimpongeza Kibaki kwa kuanzisha msingi thabiti katika elimu na maendeleo ya miundombinu na kuwa kile alichokiita mbunifu wa uchumi wa Kenya.

"Historia ya Kenya inapoandikwa, Mwai Kibaki hatafaa katika aya, hawezi kutoshea katika sura. Tunahitaji zaidi hiyo kwa kile ambacho ameifanyia nchi yetu," Ruto alisema.

Naibu rais alisema maendeleo makubwa ya miundomsingi ya Kenya ambayo tangu 2013 yameendelezwa na utawala wa Jubilee yalikuwa ni chimbuko la rais Kibaki.

"Alipanda mbegu na kuweka msingi ambao rais wetu wa nne alijenga juu yake maendeleo ya miundombinu tunayoona leo," Ruto alisema.

DP alisema kuwa hana shaka kuwa atakayekuwa rais wa tano ana maono sawa na atatafuta kuendeleza urithi wa KIbaki kuhusu miundombinu na maendeleo ya kiuchumi.

"Ni wakati mzito lakini najivunia urithi ambao tumeujenga kama taifa

"Tunaweza kupiga hatua katika siku zijazo katika msingi wa mababu zetu ikiwa ni pamoja na Mwai Kibaki. Roho yake ipumzike kwa amani," Ruto alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved