Tanzania kumuomboleza Hayati Mwai Kibaki kwa siku mbili

Muhtasari

•Rais Samia alitangaza kwamba maombolezo ya kitaifa yataanza Ijumaa, Aprili 29 hadi Jumamosi, Aprili 30.

Rais Samia Suluhu wa Tanzania
Rais Samia Suluhu wa Tanzania
Image: GOOGLE

Rais wa Tanzania Samia Hassan ametangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki.

Katika taarifa yake, Rais Samia alitangaza kwamba maombolezo ya kitaifa yataanza Ijumaa, Aprili 29 hadi Jumamosi, Aprili 30.

"Wakati wa maombolezo haya ya kitaifa ya siku mbili, bendera yetu itapandishwa nusu mlingoti ya katika maeneo yote ya nchi na balozi zote za kidiplomasia za Tanzania zilizo nje ya nchi," Rais alisema.

Rais Samia ametoa risala za rambirambi kwa wakenya na kuwataka watanzania kuwapa pole majirani wao katika kipindi hiki kigumu wanapoomboleza na rais wao wa tatu.

Rais Uhuru Kenyatta alitangaza kifo cha mtangulizi wake Ijumaa wiki iliyopita.

Hayati atazikwa siku ya Jumamosi nyumbani kwake katika eneo la Othaya, kaunti ya Nyeri.

Hafla ya mazishi ya kiserikali kwa Kibaki inafanyika leo (Ijumaa) katika Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo