Muturi atupilia mbali hati za kunyakua ardhi dhidi ya DP Ruto

Muhtasari

• Muturi alimwagiza karani wa Bunge la Kitaifa Michael Sialai kuondoa hati hizo na kumrudishia Gedi haraka iwezekanavyo. 

the star
the star

Muturi atupilia mbali hati za kunyakua ardhi dhidi ya DP Ruto  Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi mnamo siku ya Jumanne alitupilia mbali stakabadhi zilizowasilishwa na Mbunge wa Wajir Fatuma Gedi kuthibitisha madai yake kuwa naibu rais William Ruto ni mnyakuzi wa ardhi. 

Muturi alisema kwamba mbunge huyo hakufuata sheria kanuni zilizowekwa za kuwasilisha stakabadhi, na kumkosoa Gedi kwa kujaribu kumjadili Ruto kupitia mlango wa nyuma. 

Muturi alimwagiza karani wa Bunge la Kitaifa Michael Sialai kuondoa hati hizo na kumrudishia Gedi haraka iwezekanavyo. 

"Kwa kuzingatia uamuzi huu, suala hilo limefungwa na hakutakuwa na mjadala wowote kulihusu," Muturi aliagiza.  

Spika alisema utaratibu wa hoja kama hayo ni kwamba mbunge yeyote mwenye madai hayo aweke mezani nyaraka na spika athibitishe kuruhusiwa.