Uhuru akutana na Ruto katika mkutano wa baraza la mawaziri

Muhtasari

• Wawili hao walikutana katika Ikulu ya Nairobi, ambapo kiongozi wa taifa aliongoza mkutano huo.

Rais Uhuru Kenyatta akiongoza baraza la Mawaziri Alhamisi 5/12/2022
Rais Uhuru Kenyatta akiongoza baraza la Mawaziri Alhamisi 5/12/2022
Image: PSCU

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto walikutana siku ya Alhamisi kwa kikao cha Baraza la Mawaziri.

Wawili hao walikutana katika Ikulu ya Nairobi, ambapo kiongozi wa taifa aliongoza mkutano huo.

Taarifa kutoka Ikulu ilisema masuala ya umuhimu wa kitaifa na kimataifa yalikuwa yajadiliwa wakati wa mkutano huo.

"Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta leo yuko Ikulu, Nairobi, akiongoza kikao kamili cha Baraza la Mawaziri ambapo masuala kadhaa ya umuhimu wa kitaifa na kimataifa yatajadiliwa," ilisoma tweet ya ikulu.

Hii pia ni mara ya kwanza kwa Uhuru kuitisha mkutano wa baraza la mawaziri katika kipindi cha mwaka mmoja.

Baraza la Mawaziri linatarajiwa kuandaa kikao kila Alhamisi kujadili masuala muhimu yanayohusu serikali.