(+PICHA)Barabara ya Nairobi Express Way yafunguliwa kwa umma kutumia

Muhtasari
  • Barabara ya Nairobi Express Way yafunguliwa kwa umma kutumia
Barabara ya Nairobi Express Way yafunguliwa kwa umma kutumia
Image: WILFRED NYANGARESI

Barabara ya Nairobi Expressway ya kilomita 27 sasa iko wazi kwa umma.

Barabara hiyo - ambayo ni mradi mkuu wa Rais Uhuru Kenyatta - ilifunguliwa Jumamosi, Mei 14, huku wenye magari wakiruhusiwa kuitumia.

Hata hivyo, ufunguzi huo ni wa majaribio na utaruhusu waendeshaji wa barabara hiyo pamoja na serikali kuweka mianya yoyote inayohitaji kuzibwa.

Barabara ya Nairobi Express Way kuanza kutumika rasmi
Image: WILFRED NYANGARESI

Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Uchukuzi James Macharia sasa anasema Barabara ya Nairobi Expressway inayotarajiwa hatimaye iko wazi kwa matumizi ya umma.

Akizungumza Jumamosi wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo kabla ya uzinduzi huo, CS Macharia alisema kuwa hadi sasa takriban magari elfu 11,000 yamesajiliwa katika barabara hiyo, huku takriban magari 7,000 yakiwa yamesajiliwa kutumia ushuru wa kielektroniki.

Image: WILFRED NYANGARESI

Waziri huyo alisema kampuni ya Moja Expressway, iliyopewa jukumu la kusimamia barabara hiyo, imekuwa ikisajili zaidi ya magari 800 kwa siku tangu kutangaza mchakato wa usajili hivi majuzi.

Alisema Barabara ya zamani ya Mombasa itakarabatiwa kwa gharama ya Ksh.9 bilioni na itajumuisha njia ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT).

Mkandarasi huyo pia atapewa jukumu la kukarabati sehemu za barabara ambazo ziliharibika wakati wa ujenzi wa Barabara ya Expressway, na mkataba huo utasainiwa wiki ijayo.

Barabara ya Nairobi Express Way kuanza kutumika rasmi
Image: WILFRED NYANGARESI

Huku akisema kuwa Barabara hiyo ya Express inatazamiwa kupunguza msongamano wa magari katika Barabara ya Mombasa, CS Macharia aliongeza kuwa Rais Uhuru Kenyatta atasimamia uzinduzi huo rasmi wiki zijazo.

Hizi hapa baadhi ya picha za barabara hiyo na je maoni yako kuhusu barabara hiyo ni yapi?