Sherehe mjini Eldoret baada ya Gachagua kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Ruto

Muhtasari
  • Sherehe mjini Eldoret baada ya Gachagua kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Ruto
Mbunge Rigathi Gachagua na DP William Ruto
Image: Andrew Kasuku

Mkutano wa kuwaombea walioteuliwa na UDA mjini Eldoret uligeuzwa kuwa sherehe baada ya Naibu Rais William Ruto kumtaja Mbunge Rigathi Gachagua kama mgombea mwenza wake.

Mkutano wa maombi katika kituo cha TAC ulisitishwa kwa ajili ya kusambazwa moja kwa moja kwa hotuba ya DP Ruto kisha kukawa na wimbo na densi.

Wateule na maafisa wa UDA wakiongozwa na gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandago na seneta wa Kericho Harun Cheruiyot walijumuika na umati katika nyimbo na densi.

"Tuna furaha kwamba DP hatimaye alimtaja mgombea mwenza wake na tutasimama na Kenya Kwanza hadi tupate ushindi," Mandago alisema.

Mandago alisema Rigathi alistahili kuwa naibu DP Ruto, akibainisha kuwa mbunge huyo wa Mathira amethibitisha kuwa mwanachama aliyejitolea katika timu ya Kenya Kwanza.

"Amekuwa dhabiti na aliyejitolea kwa sera za kiuchumi za chini kwenda juu na amethibitisha kuwa kiongozi wa kitaifa," Mandago alisema.