Rais wa Uganda Yoweri Museveni anasema mazungumzo na mgombea urais wa Kenya, Raila Odinga yaliyofanyika Ikulu ya Entebbe yaligusia masuala yanayohusu nchi hizo mbili jirani.
Bw Odinga, ambaye anachukuliwa kuwa mmoja wa wagombeaji wa wanaoangaliwa katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, alimtembelea Rais Museveni jana jioni.
Katika ujumbe wake wa Twitter kuhusu mkutano huo, Bw Odinga alisema wamejadili historia ya pamoja ya nchi zao inayolenga kuimarisha uhusiano wa siku zijazo.
Siku mbili zilizopita, Odinga alikuwa Sudan Kusini ambako alikutana na Rais Salva Kiir na kuzindua Daraja la Uhuru la kilomita 3.6 linalotarajiwa kurahisisha usafirishaji wa bidhaa katika Mto Nile.