Marekani imeahidi zawadi ya Ksh232M kwa yeyote ambaye atatoa taarifa ambazo huenda zikafanikihakukamatwa kwa washukiwa wawili wanaosakwa kwa ulanguzi wa wanyamapori na dawa za kulevya.
Abdi Hussein Ahmed na Badru Abdulaziz wanadaiwa kusafirisha na kusambaza Kilo 190 za pembe za kifaru na tani 10 za pembe za ndovu kutoka nchi mbalimbali za Afrika hadi Marekani.
Wawili hao wanaripotiwa kushirikiana na mshukiwa wa tatu, Mandir Mohammed Suhur kutekekeza uhalifu huo katika nyakati mbalimbali kati ya Desemba 2012 na Mei 2019.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Kenya Eric Kneedler alisema pembe za faru na pembe hizo zilikuwa na thamani ya dola milioni 7 (Sh800 milioni).
Watatu hao pia wanadaiwa kusafirisha kilo kumi za Heroin kutoka Kenya hadi Marekani katika kipindi hicho.
Watatu hao walishtakiwa na Mahakama ya Wilaya ya Kusini ya Marekani ya New York mnamo Juni 14, 2019 na kufuatiwa na toleo la notisi nyekundu la INTERPOL kuhusu Suhur Mansur Mohammed na Ahmed Abdi Hussein.
Siku wa Alhamisi Mkuu wa DCI George Kinoti alifichua kuwa Badru Saleh alipatikana katika mpaka wa Busia nchini Kenya mnamo Juni 11, 2019 kisha kusafirishwa hadi Nairobi na kushtakiwa katika mahakama ya JKIA.
Badru aliachiliwa kwa dhamana ya 200,000 mnamo Julai 12, 2019 na kuagizwa kuwa anaripoti kwa wapelelezi kila baada ya siku mbili ila hajaonekana tena tangu Desemba 2019.
Kinoti amewaomba Wakenya kusaidia katika kukamwatwa kwa Abdi Ahmed na Badru hao ili waweze kufunguliwa mashtaka.
Zawadi ya Ksh 116 inatolewa kwa kila mmoja wao na Marekani (Idara ya Nchi ya Marekani, Huduma ya Samaki na Wanyamapori ya Marekani na Utawala wa Utekelezaji wa Dawa za Kulevya za Marekani), kwa usaidizi kamili wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi ya Kenya.
Yeyote ambaye ana taarifa kuwahusu ameagizwa kufahamisha wapelelezi kupitia nambari 0800722203 au ubalozi wa Marekani kupitia +18443978477.