Kibali cha Walter Mong'are kuwania urais kimebatilishwa

Muhtasari
  • Haya yanajiri wiki moja baada ya kuruhusiwa kuwania urais Jumatatu, Mei 30

Kibali cha mgombea urais Walter Mong'are kuwania kiti cha urais kimebatilishwa.

Mgombea huyo sasa amefungiwa nje ya kinyang'anyiro cha urais Agosti 9.

Haya yanajiri wiki moja baada ya kuruhusiwa kuwania urais Jumatatu, Mei 30.

Haya yanajiri pia baad ya tume ya uchaguzi IEBC kuangaza hadharani kumhoji mgombea urais huyo.

Wito huo ulikuja baada ya mgombea mwenza wa Jimi Wanjigi Willis Otieno, kuibua wasiwasi kuwa Mong'are hakupaswa kuondolewa kwa vile pia hana cheti cha shahada.

Wasiwasi ulikuja baada ya Wanjigi na mgombea mwenza wake kunyimwa kibali cha kushiriki.