Kwa nini nimezuiwa kushiriki uchaguzi? - Kigame auliza IEBC

Muhtasari
  • Mwanamuziki huyo ametilia shaka uadilifu wa IEBC akitaja kwamba alitii mahitaji yote ambayo tume hiyo iliweka
Mgombea urais Reuben Kigame akihutubia wanahabari nje ya jumba la Anniversary Tower Nairobi, baada ya jaribio lake kukutana na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kugonga mwamba./WILFRED NYANGARESI
Mgombea urais Reuben Kigame akihutubia wanahabari nje ya jumba la Anniversary Tower Nairobi, baada ya jaribio lake kukutana na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kugonga mwamba./WILFRED NYANGARESI

Mgombea Huru wa Urais Reuben Kigame amepinga Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kueleza ni kwa nini alizuiwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Agosti 9.

Akitumia ukurasa waketwitter mnamo Jumatatu, Juni 6, Kigame alieleza kwa kina matukio yaliyojiri kati ya Mei 16 alipotangazwa kwenye gazeti la serikali kama mgombea Urais hadi Mei 30 alipofungiwa nje ya kinyang'anyiro hicho.

Mwanamuziki huyo ametilia shaka uadilifu wa IEBC akitaja kwamba alitii mahitaji yote ambayo tume hiyo iliweka lakini bado akakataliwa kwa sababu zisizojulikana.

"Wakati wanaotaka kugombea wameondolewa kwa kutokuwa na saini na nakala za vitambulisho, ninazo lakini bado naonekana kutofuata sheria, marafiki kwanini nazuiwa kugombea katika uchaguzi wa Agosti? Kwa nini nchi hii inanichukulia hivi? Mtu aniambie kwa nini,"Aliuliza KIgame.