Shirika la Reli latangaza kuanza kwa safari za usiku kwenda Kisumu

Muhtasari

• Safari hizo zitakuwa kila Ijumaa na Jumapili. Mwezi Desemba mwaka 2021, kampuni ya reli ilianza safari za gari moshi kutoka Nairobi kwenda Kisumu. 

Mamlaka ya Keli ya Kenya
Mamlaka ya Keli ya Kenya
Image: Image: picha:twitter /Hisani

Shirika la Reli la Kenya limetangaza kuwa abiria sasa wanaweza kusafiri usiku kwenda na kurudi Kisumu. 

Walitoa taarifa kwenye akaunti yao ya Twitter siku ya Jumanne, iliyosema kuwa safari za usiku zitaanza Ijumaa, Juni 10. 

Abiria kutoka Nairobi wataondoka saa kumi na mbili unusu jioni na kuwasili saa kumi na mbili unusu asubuhi. 

Kwa upande mwingine, abiria mjini Kisumu watapanda gari moshi saa kumi na mbili jioni na kufika Nairobi saa kumi na mbili baadaye. 

Safari hizo zitakuwa kila Ijumaa na Jumapili. Mwezi Desemba mwaka 2021, kampuni ya reli ilianza safari za gari moshi kutoka Nairobi kwenda Kisumu. 

Muda wa kuondoka awali uliwekwa saa kumi na mbili asubuhi na muda wa kuwasili Nakuru saa tano unusu asubuhi. Safari ya kwenda Kisumu ingefika tamati saa kumi na mbili na dakika 20. 

Wakati huo, abiria walikuwa wakitozwa Shilingi 600 kwa eneo la kawaida huku eneo la watu mashuhuri likitozwa shilingi 2,000.