Aliyekuwa gavana wa Bomet Isaac Rutto ampoteza mama yake

Muhtasari
  • Aliyekuwa gavana wa Bomet Isaac Rutto ampoteza mama yake

Mamake aliyekuwa Gavana wa Bomet Isaac Rutto ameaga dunia.

Katika taarifa Jumanne, katibu mkuu wa Chama Cha Mashinani Albert Koech alisema Mama Jane Tirop alifariki alipokuwa akitibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Moi mjini Eldoret.

"Ni kwa moyo mzito kutangaza kifo cha  Mama Jane Tirop, mama mpendwa kwa Gavana Isaac Ruto, Kiongozi wa Chama cha CCM. Mama Jane alienda kuwa na Bwana Jumanne asubuhi, 14 Juni 2022 katika MTRH Eldoret, " alisema.

"Kwa niaba ya Chama Cha Mashinani, napenda kufikisha salamu za rambirambi kwa familia ya Chama chetu katika kipindi hiki kigumu."

Koech pia alitangaza kuwa chama kimesimamisha kampeni ili kuomboleza na familia ya kiongozi wao wa chama.