• Kadhi alikuwa na taaluma ya hadhi ya juu na kufanya kazi katika kampuni ya Nation Media Group kama mhariri mkuu.
Kadhi alifariki siku ya Jumatano, alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi.
Familia yake ilisema mwanahabari huyo mkongwe atazikwa Alhamisi (Leo) kwa mujibu wa imani ya Kiislamu.
Kadhi alikuwa na taaluma ya hadhi ya juu na kufanya kazi katika kampuni ya Nation Media Group kama mhariri mkuu.
Pia alikuwa msomi na alifundisha uandishi wa habari katika Chuo Kikuu cha Nairobi, Chuo Kikuu cha Addis Ababa na Chuo Kikuu cha USIU.
Kadhi, ambaye alipokea tuzo ya mafanikio ya maisha katika Tuzo za Kila Mwaka za Uandishi wa Habari za Baraza la Habari nchini (MCK) mwaka 2015, awali alikuwa mwenyekiti wa bodi ya wahariri ya jarida la Media Observer.