Je, umejipanga? Update sim details zako, ulinde sim yako

Mamlaka ya mawasiliano ilipeana hadi Oktoba 15, 2022 kwa Wakenya ambao hawajasajili laini zao kuhakikisha wamefanya vile ili kuepuka kufungiwa.

Muhtasari
  • Usajili wa sim sasa umekuwa rahisi na haraka. Ikiwa una smartphone, sasa kusajili sim yako ni rahisi kama kubonyeza *106*2#. Baada ya hapo, chagua  usajili wa sasisho.
  • Ikiwa huna smartphone, basi tembelea tu Duka la Safaricom lililo karibu nawe,au agent ama dealer na uhakikishe umebeba Kitambulisho chako cha Taifa ili kukamilisha usajili.

Safaricom inawahamasisha wateja wake kuendelea kufanya juhudi kuhakikisha kwamba wamesajili laini zao za simu huku muda wa makataa uliotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (CA) ukiwa umebakisha chini ya miezi minne.

Mamlaka ya mawasiliano ilipeana hadi Oktoba 15, 2022 kwa Wakenya ambao hawajasajili laini zao kuhakikisha wamefanya vile ili kuepuka kufungiwa.

Mwanabiashara Amina Nzau anayefanya kazi kwa duka la dawa, alitueleza kwamba kusajili sim yake ilikuwa rahisi sana. “Nilitembelea duka la Safaricom lililoko TRM, nilikuwa nimebeba kitambulisho cha taifa, nikajitambulisha, nikapigwa picha na kujisajili, kisha nikaondoka baada ya muda mchache, sikupiga foleni wala kulipa chochote,” mfanyi biashara huyo alisema.  Nzau amawahimiza Wakenya kujipanga na kwenda kusajili sim zao, wasiogope.

Usajili wa sim sasa umekuwa rahisi na haraka. Ikiwa una smartphone, sasa kusajili sim yako ni rahisi kama kubonyeza *106*2#. Baada ya hapo, chagua  usajili wa sasisho.

Utapokea ujumbe kwa rununu yako na tovuti ya Safaricom https://Safaricom.com/account/kyc-upload. Mara tu unapobofya tovuti hiyo, sasisha maelezo yako na upakie nyaraka zako ili kujidhibitisha. Hii inafanya kazi kwa wale walio na smartphones ambazo zimewezeshwa na mtandao.

Ikiwa huna smartphone, basi tembelea tu Duka la Safaricom lililo karibu nawe,au agent ama dealer na uhakikishe umebeba Kitambulisho chako cha Taifa, Kitambulisho cha Alien au Pasipoti ili kukamilisha usajili.

Kumbuka kusajili sim ni rahisi na kwa hiari yako na ni bure, haulipi chochote. Hata hivyo, ni muhimu sana kwani inakulinda dhidi ya wadanganyifu ambao huiba vitambulisho kufanya uhalifu na vitendo vingine visivyo halali kama vile magaidi.

Update sim details ulinde sim yako!