Maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani

Nchini Kenya siku hiyo inaadhimishwa kwa matembezi yakiongozwa na waziri wa Utalii na Wanyama pori Najib Balala.

Muhtasari

• Nchi za Afrika zinazofunza Kiswahili shuleni ni Kenya, Tanzania, Rwanda, Uganda, Somalia, Kongo DRC, Sudan Kusini, Afrika Kusini, Botswana, Ethiopia, Namibia, Malawi-Mozambique na Burundi.

Waziri wa Utalii Najib Balala kuongoza maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani.
Waziri wa utalii Najib Balala Waziri wa Utalii Najib Balala kuongoza maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani.
Image: Fredrick Omondi

Leo ni maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani.

Kenya ilijiunga rasmi na mataifa mengine barani Afrika yanozungumza lugha ya Kiswahili katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili.

Tarehe saba Julai ilitengwa kuwa siku rasmi ya kusherehekea lugha hiyo na Shirika la Umoja wa Mataifa mnamo Novemba Mwaka Jana.

Kiswahili ndio lugha ya pekee ya Kiafrika ambayo imetambulika na Umoja wa Mataifa.

 Waziri wa Utalii Najib  Balala, akiongoza maadhimisho ya sherehe hizo jijini Nairobi, aliwaagiza wakenya wajivunie umaarufu wa lugha ya Kiswahili kwa Kuizungumza  na kujifunza, kama ishara ya uzalendo kwa nchi ya Kenya.

Kiswahili kimeorodheshwa na majarida mbali mbali kama lugha inayokuwa kwa kasi mno kote duniani huku nchi kadhaa za Afrika Mashariki zikitangaza kutumia lugha hiyo kama lugha rasmi ya mataifa hayo.

Nchi zinazongoza kwa matumizi ya Kiswahili ni Tanzania, Kenya na Uganda.

Nchi za Afrika zinazofunza Kiswahili shuleni ni Kenya, Tanzania, Rwanda, Uganda, Somalia, Kongo DRC, Sudan Kusini, Afrika Kusini, Botswana, Ethiopia, Namibia, Malawi-Mozambique na Burundi.

Sherehe pia inafanyika mjini Mombasa.