Jamaa afariki baada ya kubugia pombe kwenye mashindano ya unywaji

Jamaa huyo alibugia pombe hiyo kali kiasi cha mililita 750 chini ya dakika mbili na kufqariki muda mfupi baadae

Muhtasari

•Mashindano ya Unywaji Pombe umesababisha kifo.

•Tukio hilo lilifanyika Afrika Kusini.



Jamaa aliyebugia pombe hadi kufa Afrika Kusini
Jamaa aliyebugia pombe hadi kufa Afrika Kusini
Image: Screenshot

Kijana mmoja kutoka nchini Afrika Kusini alifariki baada ya kukunywa pombe  aina  Jagarmeister kwa chini ya dakika mbili kwenye mashindano ya unywaji pombe.

Mwendazake alionekana  kwenye video iliyosambaa kwenye mitandao akibugia kinywaji hicho huku watu wakimshangalia.

Tukio hili ilifanyika katika mojawapo ya maeneo ya kuuza pombe za kienyeji huko Waterval Limpopo, Afrika Kusini.

Pesa takriban Randi mia mbili  ambazo ni sawa na  Ksh.1,400 za Kenya  zilitengwa kama zawadi kwa yule ambaye angeshinda katika shindano hilo.

''Mshindi ambaye anaweza kukunywa haya pombe kwa kutumia muda mfupi mno atapata zawadi ya Pesa R 200''  moja ya vyombo vya habari ilidaiwa kuwa Bw. Majopelo alisema.

Kijana huyo mwenye umri kati ya (25-30)  alikimbizwa hospitalini  na baada ya muda mfupi akatangazwa kuwa amefariki.

"Ni kitu cha kushangaza  sana... kwani... hii sio  kitu cha kuchekesha hata kidogo ... ulikuwa mchezo ambao haukuwa sawa kutoka pande zote kwa mwaadhiriwa pamoja na yule ambaye aliandaa ile mashindano," Mteja mmoja alitoa maoni yake.

Kinywaji hicho chenye kiwango cha 750ml  ya Kijerumani kilichotengenezwa kwa mimea na viungo  tofauti  kina pombe kwa kiwango cha asilimia 35.

Polisi wa Limpopo sasa wameanza uchunguzi kuhusu kile ambacho kinadaiwa uenda kilisababisha kifo cha huyo Kijana.