Jacque Maribe akiri kosa la pili

Mahakama pia ilisema Maribe, ambaye ndiye mwandishi wa taarifa hiyo, hakuwa amepinga taarifa hiyo kuwasilishwa.

Muhtasari

•Jacque Maribe aliyeambatana na wakili wake Katwa Kigen anadaiwa kumfungukia Otieno na kumwambia kuwa anataka kubadilisha kauli yake na kusema kilichotokea.

Joseph Irungu akiwa ameshika bunduki ya kivita akiwa na jeraha la risasi. Mfanyabiashara aliyeuawa Monicah Kimani
Joseph Irungu akiwa ameshika bunduki ya kivita akiwa na jeraha la risasi. Mfanyabiashara aliyeuawa Monicah Kimani
Image: MPASHO

Joseph Irungu almaarufu Jowie mnamo Jumanne alipoteza ombi la kusimamisha upande wa mashtaka kutoa taarifa ya Jacque Maribe inayomhusisha na kesi ya mauaji.

Jowie, kupitia wakili wake Hassan Nandwa, alikuwa amepinga kutolewa kwa taarifa hiyo iliyoandikwa na Maribe ambapo aliwaambia polisi kwamba yeye (Jowie) alijipiga risasi nyumbani kwake.

Nandwa alisema kauli hiyo ni ya kukiri kosa na inapaswa kuchukuliwa hivyo akimaanisha kwamba taarifa hiyo ilipaswa kufuata utaratibu sahihi wakati inachukuliwa.

Inspekta mkuu Maxwell Otieno alikuwa ameambia mahakama kwamba taarifa aliyochukua kutoka kwa Maribe ilikuwa ya pili kurekodi akiwa na polisi.

Hapo awali Maribe alikuwa amerekodi taarifa yake ya kwanza ambayo ilithibitisha taarifa ya Jowie lakini Septemba 29 aliamua kwa hiari kuibadilisha hivyo kauli ya pili.

Katika uamuzi mfupi, Jaji Grace Nzioka aliruhusu upande wa mashtaka kutoa maelezo ya pili ya Maribe, akisema haitakuwa inatumika  kwa Jowie.

Hakimu Nzioka alisema upande wa mashtaka ulithibitisha kwamba taarifa hiyo haikuwa ya Maribe kama ilivyodaiwa.

 

"Sheria iko wazi jinsi taarifa ya washukiwa dhidi ya mwingine inavyochukuliwa. Hata ikikubaliwa, hatabaguliwa kwani atapata fursa ya kuichunguza,” hakimu akaamua.

Mahakama pia ilisema Maribe, ambaye ndiye mwandishi wa taarifa hiyo, hakuwa amepinga taarifa hiyo kuwasilishwa.