KNEC yaonya Wakenya dhidi ya tangazo potovu la kazi kwa watahini

Walitaka walimu hao kulipa ada ya mafunzo ya Sh10,500

Muhtasari

•Katika taarifa iliyotolewa Julai 21, Wizara hiyo ilifanya haraka kuwaonya umma juu ya hilo.

•"Tangazo hilo linasambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Si halali," KNEC ilibaini.

Makao makuu ya KNEC kwenye nyumba ya mitihani.
Makao makuu ya KNEC kwenye nyumba ya mitihani.
Image: STAR

Baraza la Kitaifa la Mitihani la Kenya limewaonya Wakenya dhidi ya habari potovu, haswa kwenye mitandao ya kijamii.

Baraza hilo limesema hayo baada ya kuarifiwa kuwa kuna habari  inayosambazwa  kwenye mitandao ya kijamii ikisema walimu wanatakiwa kupewa mafunzo ya maandalizi ya mitihani ya taifa.

Katika taarifa iliyotolewa Julai 21, Baraza hilo lilifanya juhudi za haraka kuwaonya umma juu ya hilo taarifa potovu.

"Tangazo hilo linalosambazwa kwenye mitandao ya kijamii. si ya ukweli," KNEC ilibaini.

Taarifa huo ulikuwa umewataka walimu hao kulipa ada ya mafunzo ya Sh10,500 kupitia huduma za pesa kwa njia ya simu.

"Kila mwalimu kulipa ada ya mafunzo ya Sh10,500 kupitia bili ya malipo ya KNEC nambari 819313 kwa kutumia nambari yake ya simu iliyosajiliwa" sehemu ya ujumbe huo uliosambazwa .

Walimu hao  walitakiwa kutaja eneo lao la mafunzo yaani KCPE, KCSE, PTE, DTE, Biashara au mafunzo ya kiufundi.

"Walimu watakao faulu watafunzwa kusahihisha mitihani, na pia  watajumuishwa katika hifadhidata ya Watahini wa KNEC," ilisoma sehemu ya chapisho lililosambazwa.

Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi hayo, kwa mujibu wa barua hiyo feki, ilisomwa Septemba 2022, huku mafunzo hayo yakipangwa kati ya Oktoba 3 na Oktoba 9.

KNEC iliwaonya Wakenya kuhusu habari hizo feki, ikitaja kuwa habari sahihi kutoka kwa tume hiyo inachapisha kwenye kurasa zake rasmi pekee.

Mtihani wa KCPE utafanywa kuanzia Novemba 28 hadi Desemba 1, huku KCSE ikifanywa kuanzia Desemba 1 hadi Desemba 23.

Mchakato wa kusahisha  mtihani hizo utafanywa kuanzia Januari 2, 2022 hadi Januari 20, 2022.