Abiria wa kigeni aliyekamatwa na vibandiko vya IEBC aachiliwa

Uchunguzi umebaini kuwa stika hizo ni mali ya IEBC

Muhtasari

•Abiria alikuwa na roli 17 za stika za majimbo mbalimbali nchini.

•Roli zilinaswa na msafiri alizuiliwa kwa kuulizwa maswali.

Msemaji wa polisi Bruno Shioso.
Msemaji wa polisi Bruno Shioso.
Image: STAR

Abiria  wa kigeni ambaye Alhamisi alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) akiwa na stika za uchaguzi za IEBC ameachiliwa kutoka kizuizini.

Siku ya Alhamisi, maafisa wa upelelezi kutoka DCI walianza uchunguzi baada ya lebo za shirika la uchaguzi kunaswa kutoka kwa abiria ambaye alikuwa amezificha kwenye begi lake la kusafiria.

Abiria huyo alikuwa na roli 17 za stika za majimbo mbalimbali ya uchaguzi nchini.

Shioso pia alisema kuwa vibandiko hivyo havikuandamana na afisa wa IEBC kulingana na utaratibu wa kawaida na havikutangazwa kwa mujibu wa sheria.

"Polisi, kulingana na utaratibu na mpangilio wa kawaida na IEBC, hawakuarifiwa kuhusu uagizaji kama huo mapema ili kutoa usalama muhimu na kusindikiza," akaongeza.

Vifaa hizo na mshukiwa zilizuiliwa huku akisubiri kuulizwa maswali kuzihusu.

Baadaye alipelekwa katika makao makuu ya DCI ambako alikaa sehemu nzuri zaidi ya siku.

Katika uchunguzi wao, polisi walitaka kuelewa kwa nini abiria alikuwa amebeba vifaa hivyo na ni nani aliyempa.

Msemaji wa NPS Bruno Shioso alisema uchunguzi umebaini kuwa stika zilizopatikana ni mali ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

"Kukamatwa, kuzuiliwa  kwake ni kwa sababu ya kumiliki  vifaa vya uchunguzi " alisema.

Kufuatia uchunguzi huo, mshukiwa aliachiliwa baadaye na stika kukabidhiwa IEBC.